Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda
akimkabidhi bahasha yenye hundi ya malipo ya Ada ya shule na matumizi ya msingi
kwaajili ya masomo yake, kwa mmoja wa wanafunzi aliyenufaika ufadhili huo,
(kulia) Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Bw. Khalfan Abdulrahman
Al-Mazouqi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa
katika picha ya pamoja na wanafunzi wanufaika wa ufadhili wa kulipiwa Ada ya
Kidato Cha Tano na Sita kwa Watoto wa Kike 100 Kutoka Familia Duni Waliofaulu
Masomo ya Sayansi na Kushindwa kuendelea na Masomo kwa kukosa Ada.
Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Bw. Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi akimkabidhi bahasha yenye hundi ya malipo ya Ada ya shule na matumizi ya msingi kwaajili ya masomo yake, kwa mmoja wa wanafunzi aliyenufaika ufadhili huo.
Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Bw. Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi akimkabidhi bahasha yenye hundi ya malipo ya Ada ya shule na matumizi ya msingi kwaajili ya masomo yake, kwa mmoja wa mzazizi wa mwanafunzi aliyenufaika ufadhili huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wanufaika wa ufadhili wa kulipiwa Ada ya Kidato Cha Tano na Sita kwa Watoto wa Kike 100 Kutoka Familia Duni Waliofaulu Masomo ya Sayansi na Kushindwa kuendelea na Masomo kwa kukosa Ada.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul
Makonda September 17 ametimiza ahadi ya ufadhili wa Masomo kuanzia Kidato cha
Tano hadi Sita kwa Watoto wa kike 100 kutoka familia duni waliofaulu masomo ya
Sayansi lakini wakashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa Ada ambapo katika
ufadhili huo amewalipia Ada na Vifaa ya shule ikiwemo Sare, mabegi, vitabu,
madaftari na Nauli.
RC Makonda amesema lengo la ufadhili huo ni
kumkomboa mtoto wa Kike kutoka familia duni aweze kupata elimu bora
itakayosaidia kubadili maisha ya Familia na mwisho wa siku kuwa na Taifa lenye
Wanawake Wanasayansi na Wagunduzi.
Aidha RC Makonda amesema ufadhili huo unaenda
sambamba pia na kumuunga Mkono Rais Dkt.John Magufuli alieamua kumkomboa mtoto
wa mnyonge kwa kutoa elimu bure kuanzia Darasa la Kwanza hadi kidato cha nne na
yeye ameamua kupokea kijiti kwa kuwasomesha kidato cha tano na Sita ili
wakifika vyuo vikuu wanufaike na Mkopo.
Hata hivyo RC Makonda amesema zoezi hilo
litakuwa endelevu kila mwaka ambapo amewahimiza wanafunzi waliobahatika kupata
fursa hiyo waitumie vizuri huku akimshukuru Balozi kwa Kumuunga mkono katika
kampeni hiyo.
Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Falme za
Kiarabu UAE Bw. Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi amesema ufadhili huo ni
Mwendelezo wa Kuunga Mkono juhudi za RC Makonda kwenye kila jambo kwakuwa
amekuwa mtu wa kupigania maslahi ya Wananchi anaowaongoza.
No comments:
Post a Comment