Waziri Atoa Mwezi Mmoja Mfumo Wa Mipaka Kufanya Kazi - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, June 7, 2024

Waziri Atoa Mwezi Mmoja Mfumo Wa Mipaka Kufanya Kazi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na askari wa idara ya uhamiaji ya nchini Burundi wakati wa ziara ya ukaguzi wa Mpaka wa Manyovu unaotenganisha nchi ya Tanzania na Burundi. Waziri Masauni yuko katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma.
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Nhayalina akimuonyesha eneo lililovamiwa na raia wa Burundi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua Mpaka wa Manyovu unaotenganisha nchi ya Tanzania na Burundi. Wengine ni ujumbe ulioongozana na Waziri Masauni katika ziara hiyo mkoani Kigoma.

Na Mwandishi Wetu, Manyovu

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ametoa mwezi mmoja kwa Idara ya Uhamiaji nchini kuhakikisha Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mipaka kufanya kazi katika Kituo cha Uhamiaji Manyovu ili kuepusha upotevu wa mapato ya nchi,kuepusha mifumo ya rushwa na kudhibiti uingiaji wa watu wanaoweza kuhatarisha amani ya nchi.

Ametoa kauli hiyo baada ya kukagua shughuli za uingiaji na utokaji wa raia na wageni wanaokwenda nchini Burundi kupitia Kituo cha Uhamiaji Manyovu kilichopo katika Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambapo pia amewataka kuhakikisha wanadhibiti vipenyo mbalimbali vinavyopatikana katika mpaka huo.

"Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama na hilo ameshalitekeleza na mtaona jinsi alivyowapandisha vyeo askari wa ngazi mbalimbali lakini sasa wajibu uenda sambamba na haki kwahiyo lazima muongeze jitihada katika kufanya kazi zenu, haiwezekani Waziri ndio aje hapa kufuatilia suala la mfumo, mara sijui mfumo wa kiyoyozi aufanyi kazi, sasa nishamuelekeza Kamishna Jenerali kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja mfumo huo unafanya kazi,haiwezekani serikali imewekeza fedha nyingi katika mfumo huu wa uhamiaji mtandao sasa haiwezekani leo usiwe unafanya kazi mnakaa kubeba fedha za wananchi na kuzipeleka benki kwa njia ya kawaida" alisema Waziri Masauni.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Mfawidhi wa Kituo cha Manyovu,Inspekta Arnold Masha aliweka wazi hali ya uingiaji na utokaji wa wageni kupitia kituo hicho ambapo jumla ya wageni na raia wa Tanzania 38624 waliingia na kutoka nchini kupitia mpaka wa Manyovu na jumla ya wakimbizi rai awa Burundi 3667 walipita katika mpaka huo wakirejea nchini kwao kwa hiari tangu Machi mpaka Mei 2024 huku Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Kanali Michael Nhayalina akiahidi kuimarisha utendaji na kuyafanyia kazi maagizo ya serikali yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages