Katika kuleta ufanisi na ubunifu kwenye sekta ya Mawasiliano,
ambayo imeleta mabadiliko kwenye maisha ya mamilioni ya Watanzania, Kampuni ya
mawasiliano Zantel imeendelea kuboresha huduma za kisasa za mtandao wake ili
kuhakikisha wateja wao wanazidi kufurahia huduma ya mtandao wenye kasi wa 4G.
Uboreshaji unaoendelea utaweza kuhimarisha zaidi ubora wa
mtandao wetu, huduma za intaneti za kasi zinazotumiwa zaidi kwa sasa sokoni na
wateja ni hii ya 4G.”
Aidha, aliongeza kwa kusema, Uboreshaji wa maeneo yote ya
Stone Town na mikoa ya Magharibi umefanikiwa. Zoezi la kuendelea kuboresha
huduma hizo kwa visiwa vya Unguja na Pemba linaendelea na litakamilika ifikapo
Mei mwaka huu.
Mradi mzima utagharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 10
hadi kukamilika. Mtandao wa Zantel utaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja
wake, pamoja na mtandao utakaowafikia zaidi ya asilimia 85 ya Watanzania
wanaotumia huduma za simu ya mkononi zenye ubora zaidi, intaneti yenye kasi
pamoja na kuboresha huduma za fedha.
Amesema mradi una lengo kufanya mabadiliko kwenye vituo vyote
vya huduma za katika mitandao ya simu kwa kisiwa cha Zanzibar na Tanzania Bara
kwa kufunga vifaa bora vya kisasa.
Mtandao wa Zantel unawakaribisha Watanzania wote kutumia na kufurahia
huduma ya intarneti ya 4G kutoka Zantel kama kampuni ya mtandao wa simu ya
kwanza kuleta huduma za kibenki kwa jamii ya Kiislamu na kwa nchi nzima.
Kuhusu
Zantel
Mtandao
wa Mawasiliano wa Zanzibar (Zantel) ni miongoni mwa wawekezaji na wagunduzi
kwenye sekta ya mawasilino wakiongoza kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Lakini zaidi ya yote, ni miongoni mwa kampuni ya mawasilino inayokuwa kwa kasi
kubwa na inayotengeneza faida kubwa katika Sekta ya mawasiliano Tanzania.
Mtandao huu wa Mawasiliano Zanzibar ndiyo mtandao pekee wa huduma za mawasilino
unaotoa huduma ya simu za nje kwa bei nafuu, simu bando kupitia mfumo bora wa
CDMA, GSM, 3G networks.
Huduma za
Zantel zimekuwa zikikua kutokana na kuongezeka watumiaji wake huku ikizidi
kuonyesha ubora katika huduma zake ambazo kila mtu anaweza kuzimudu pamoja na
kutoa huduma ya haraka ya mtandao wa wireles kwa haraka na ubora.
Zantel
imepokea tuzo mbalimbali kutokana na kutambuliwa kutoa huduma bora na ufumbuzi
kwenye sekta ya mawasilino. Baadhi yake ni pamoja na Tuzo ya GSMA M – Health.
Zantel imedhamiria kuwaunganisha watu ulimwenguni ili wawe mstari wa mbele
kupata tarifa kwa haraka.
Kwa
maelezo zaidi tafadhali, tembelea mtandao wetu…www.zantel.com
No comments:
Post a Comment